Public Relations Society of Tanzania

Matumizi ya Bima

Matumizi ya Bima

PUBLIC RELATIONS SOCIETY OF TANZANIA TAARIFA KWA WANACHAMA KUANZA MATUMIZI YA BIMA YA NISHIKE MKONO

Ndugu wanachama, uongozi wa Public Relations Society of Tanzania (PRST) umefanya utafiti katika benki kadhaa hapa nchini juu ya bima ya mazishi maarufu kama (BIMA YA NISHIKE MKONO) na kuona kuwa kuna umuhimu kwa wanachama wote kujiunga na huduma ya bima ya nishike mkono katika benki ya Tanzania Commercial Bank (TCB). Uamuzi wa kujiunga na huduma katika benki ya TCB unatokana na masharti na mafao yanayotolewa ukilinganisha na benki nyingine. Hivyo, PRST inawasihi wanachama wake wote kujiunga na huduma hii ili kuepusha usumbufu na ugumu wa kuchangisha rambirambi mara mwanachama anapopatwa na msiba. Mfumo wa awali wa rambirambi ulijikita kwa mwanachama tu lakini mfumo wa bima umejumuisha wategemezi muhimu wote. Pia, kiasi kinachopatikana wakati wa rambirambi huwa ni kidogo sana ukilinganisha na kiasi kinachotolewa na bima ya nishike mkono. Kwa taarifa hii, PRST haitahusika kwa namna yoyote kuchangisha rambirambi badala yake itahakikisha mwanachama anapata fao lake kwa mujibu wa utaratibu wa huduma hii ambayo malipo hufanyika ndani ya masaa 24. Kulingana na utaratibu, wanachama wanapaswa kuchagua aina moja ya bima ambapo wanachama wote watajiunga na aina hiyo kama inayoonekana katika jedwali hapo chini.

Ndege Makura,

KATIBU MKUU.

secgen@prst.or.tz 05.03.202

Share This

Comments